Tunapenda kuwajulisha kuhusu maboresho yanayokuja katika ratiba ya malipo ya huduma zinazolipiwa kwa vipindi vya kila mwezi za FellaHost Company Limited.
Katika kuendelea kuboresha uwazi, utaratibu na urahisi wa usimamizi wa malipo, ratiba maalum kwa huduma zenye kuhusisha malipo ya kila mwezi, ambapo tarehe ya kawaida ya malipo na kufanya upya huduma itakuwa tarehe 1 ya kila mwezi.
Nini kinabadilika?
Kwa mujibu wa ratiba mpya:
-
Tarehe za malipo ya huduma zinazorudiwa zitawekwa kuwa tarehe 1 ya kila mwezi.
-
Ankara (invoice) zitatolewa kwa kawaida siku 3 kabla ya tarehe ya malipo.
-
Huduma mpya zitakazoanzishwa katikati ya mwezi zitatozwa kwa utaratibu wa Prorata Billing.
-
Prorata Billing ina maana kwamba mteja atalipia kipindi halisi cha huduma anachopokea kabla ya kuingia kwenye ratiba ya kawaida ya malipo ya tarehe 1 ya kila mwezi.
-
Kipindi chochote cha huduma ambacho bado hakijalipiwa kitaingizwa kwenye ankara husika ili huduma iweze kuendana na tarehe mpya ya malipo ya kila mwezi.
Hakuna Ongezeko la Bei za Huduma
Tunapenda kusisitiza kwamba mabadiliko haya hayahusishi ongezeko la bei za huduma kwenye huduma.
Hakutakuwa na ongezeko la gharama za huduma zako kutokana na mabadiliko haya. Kinachobadilika ni muda na mpangilio wa kufanya malipo, ambapo malipo ya huduma zinazorudiwa yataunganishwa na kuwa na tarehe ya kawaida ya malipo ya tarehe 1 ya kila mwezi.
Prorata Billing, imeanzishwa ili kuwezesha mpangilio huu kwa haki na uwazi, kwa kuhakikisha kuwa mteja anatozwa kulingana na kipindi halisi cha huduma anachopokea.
Hii ina maana gani kwako?
Kuanzia utekelezaji wa ratiba hii mpya utakao anza September 01, 2026 ankara (invoice) zako za huduma zinazorudiwa kwa kila mwezi zitafuata ratiba rahisi na inayotabirika, ambapo tarehe 1 ya kila mwezi itakuwa tarehe ya kawaida ya kufanya upya huduma na malipo.
Kwa sasa huhitaji kuchukua hatua yoyote. Huduma zako zitaendelea kufanya kazi kama kawaida, na ankara zitaendelea kupatikana kupitia njia za kawaida za FellaHost.
Tunashukuru kwa kuendelea kuiamini FellaHost na tutaendelea kuboresha uwazi, ufanisi na ubora wa huduma tunazokupatia. Maboresho haya yamezingatia sera ya utoaji huduma na faragha, ili kudhibiti ubora na ufanisi wa utoaji huduma zetubila kuvunja haki za watumiaji wa huduma zetu.
Kwa heshima,
FellaHost Company Limited
Huduma kwa Wateja
www.fellahost.co.tz